Azam fc leo walikuwa ugenini katika uwanja wa shekhe Amri Abeid uliopo Arusha ilibidi wangoje mpaka dakika ya 43 kupata goli hilo pekee la ushindi likiwa limetiwa kimiani na Abdallah Seif.
Dakika mbili mbele baada ya goli hilo kuingia, kiungo Jabir Azizi alizawadiwa kadi nyekundu na mchezo kwenda mapumziko kwa azam fc wakiwa mbele kwa goli 1-0, ambapo liliendelea kudumu mpaka mwisho wa mchezo.
Azam fc wamemaliza ligi wakiwa na pointi 54 na kuwa nafasi ya pili ambapo mwakani watapata nafasi ya kushiriki katika michuano ya kombe la shirikisho.
Kiungo wa azam fc Ibrahim Mwaipopo alitwawazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo wa leo.
0 Maoni:
Post a Comment