Wednesday, May 15, 2013

BAADA YA KAZI NZITO, WAKIMATAIFA WATANGULIA KULA LIKIZO

Posted By: Unknown - 8:42 AM

Share

& Comment

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kuifikisha azam fc katika hatua ya tatu katika kombe la shirikisho na kuipa uhakika ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho mwakani, wachezaji wa 5 wakimataifa wa azam fc wame kuwa wa mwanzo kuanza likizo ya mwisho wa msimu unaotaraji kumalizika mei 18 mwaka huu.

Wachezaji hao ni Joackins Atudo na Humphrey Mieno toka Kenya, Brian Umonyi toka Uganda na Waivory coast Kipre Tchetche na Michael Bolou wamepewa ruhusa ya kurejea kwao kwa ajili ya kuanza likizo kukiwa bado kuna mchezo mmoja dhidi ya JKT Oljoro.

Msemaji wa azam fc Japhari Iddi Maganga amesema kuwa wachezaji hao watano wamepewa likizo na hawata kuwemo katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya JKT Oljoro.

Maganga amesema kuwa kocha Stewart Hall atawatumia wachezaji wake wa ndani kati mchezo huo utaka6 chezwa jijini Arusha siku ya jumamosi.

Azam teyari wameshajihakikishia nafasi ya pili ambayo inawapa nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho, na kupelekea mchezo huo wa mwisho kuwa wa kukamilisha ratiba.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.