Makamu bingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC wameanza vibaya msimu
mpya wa ligi kuu ya vodacom baada yak uwambulia sare ya goli 1-1 toka
kwa wakatamiwa wa Turiani Mtibwa sugar mchezo uliochezwa katika uwanja
wa Manungu Complex.
Katika mchezo huo ambao Mtibwa
sugar waliutawala na kuipa kazi ya ziada ngome ya Azam FC walikuwa wa
mwanzo kupata goli katika dakika ya 6 kupitia kwa mshambuliaji wao
chipukizi Juma Lizao akiunga vyema pande la kiungo mchezeshaji wazamani
wa SC Villa na Simba SC Shabani Kisiga.
Goli hilo
liliendelea kuwapa nguvu Mtibwa sugar ya kulishambulia lango la Azam FC
lakini jitihada ya mlinda mlango kinda Aishi Manula pamoja na safu yake
ya ulinzi iliweza kuondosha hatari hizo.
Azam FC
walisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati uliopigwa na beki Aggrey
Morice na kupelekea mchezo kwenda mapumziko milango ikisomeka 1-1.
Azam
FC walianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ambapo aliingi
Kipre Bolue katika nafaci ya Himid Mao na Khamisi Mcha katika nafasi ya
Ibrahim Mwaipopo mabadiliko ambayo yalipelekea timu hizo kushambuliani
kwa zamu.
Katika dakika mbili za nyongeza kama Azam FC
wangekuwa makini wangeweza kupata goli la ushindi baada ya kulisaka
lango la Mtibwa Sugar kwa dakika zote mbili ikiwa Mtibwa Sugar wakitokea
kupoteza nafasi kupitia kwa Mussa Mgosi, na kupelekea mchezo kumalizika
kwa sare ya goli 1-1
Saturday, August 24, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment