Na Mahmoud Zubeiry, Tabora BIN ZUBEIRY
KIKOSI cha Azam FC kimewasili usiku jana (jumapili agosti 25) mjini Tabora, kikitokea Morogoro tayari kwa mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumatano dhidi ya wenyeji, Rhino Rangers Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini hapa.
Azam imefika majira ya saa 4:30 tangu iondoke asubuhi mjini Morogoro na imefikia katika hoteli ya Mwafrika, jirani kabisa na Uwanja wa Mwinyi.
Meneja
wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari amesema timu itapumzika kutwa ya
kesho na jioni itafanya mazoezi, kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa
kwa hamu na wakazi wa mjini hapa.
Azam ilianza Ligi Kuu kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar jana kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
![]() |
Wako Mboka Manyema; Wachezaji wa Azam kulia John Bocco, Erasto Nyoni katikati na kushoto Said Mourad |
Azam ilianza Ligi Kuu kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar jana kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Mtibwa
walitangulia kupata bao kupitia kwa Juma Luizio dakika ya nne kabla ya
Aggrey Morris kuisawazishia Azam kwa penalti dakika ya 19.
Baada
ya mechi hiyo, Azam inayofundishwa na kocha Muingereza, Stewart Hall
ilikwenda kulala mjini Morogoro na asubuhi wakaondoka na basi lao kubwa
la kisasa kuja Tabora, walipofika usiku huu.
Rhino,
inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) iliyopanda Ligi Kuu
msimu huu, nayo ilianza Ligi Kuu kwa sare ya kufungana 2-2 na Simba SC
jana Mwinyi.
0 Maoni:
Post a Comment