Monday, August 5, 2013

AZAM KUCHEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA LEO

Posted By: azam fans - 8:34 AM

Share

& Comment

Mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la mapinduzi Azam fc wanataraji kucheza mchezo wake wa kwanza katika ardhi ya South Afrika toka ianzishwe.

Azam fc watacheza na Kaizar Ciief, ukiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania inayotazamiwa kuanza agosti 24 mwaka huu.

Washindi wapili mara mbili mfululizo, Azam fc walitua Afrika kusini siku ya jumamosi na jana wakafanya mazoezi ambapo leo watacheza mcheza wa kwanza katika ziara yao ya juma moja nchini humo.

Azam fc safari hii wa meamuwa kuweka kambi Afrika kusini baada ya kuwa na kambi ya manufaa katika misimu miwili mfululizo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati ambapo wamefanikiwa kuhodhi nafasi ya pil4 katika msimamo wa ligi kuu mara mbili mfululizo na kutwa kombe la mapinduzi mara mbili mfululizo na kufanikiwa kufika fainali katika kombe la Kagame (klabu bingwa Afrika mashariki na kati).

Azam fc wametua Afrika kusini na kikosi chake chote isipokuwa Mganda Brian Umonyi na Mkenya Humphrey Mieno walio majeruhi.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.