Timu ya Azam FC inapenda kuwatangazia Wazazi na Walezi wote wenye nia ya kuleta Watoto wo kwenye Majaribio ya kila mwezi ambayo huwa yanafanyika kila Tarehe Mosi ya Mwezi kwamba, kutokana na sababu za Kiufundi na Kiutawala, majaribbio ya mwezi Novemba yatafanyika Tarehe 2 Novemba 2013 saa 1 asubuhi mapema ambayo itakuwa ni siku ya Jumamosi. Tunapenda kuwataarifu pia kwamba Watoto watakaohusika na zoezi hili ni wale wenye umri wa miaka 16 kushuka chini, kwa lugha nyepesi ambayo imezoeleka ni Under 17.
Wale wote ambao hawana hiyo sifa kuu ya U17 tunawaomba radhi wasijisumbue kufika kwani hatutawapokea kabisa. Kwasasa Klabu ina vijana wengi wa U20 ambao tayari wapo kambini.
Tumeamua kufanya zoezi hili Jumamosi tukiamini kwamba U17 wengi ni wanafunzi kwahiyo tarehe 1 Novemba ambayo ni Ijumaa wengi wao kama sio wote watakuwa shuleni.Tafadhali Mtoto awe ana miaka 16 kushuka chini, yani waliozaliwa kuanzia tarehe 1.1.1998 na kuendelea na wala sio vinginevyo.
By Utawala.
Wednesday, October 30, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment