Mshambuliaji
wa Ruvu Shooting ,Juma Hamisi (kushoto) akiwania mpira na
Winga wa Azam Fc,Khamis Mcha, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara
uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Chamanz i jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Azam Fc wakishangilia bao la
pili lililofungwa na Joseph Kimwaga dhidi ya Ruvu
Shooting katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Mshambuliaji wa Ruvu
Shooting ,Juma Hamisi (kushoto) akiwania mpira na Winga wa Azam Fc,Khamis Mcha,
katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara ulichezwa kwenye Uwanja wa Chamanzi
jijini Dar es Salaam.
Picha na Francis Dande
Picha na Francis Dande
Mabingwa wa kombe la mapinduzi na washindi wa pili wa ligi kuu ya vodacom msimu uliopita Azam FC leo wamefanikiwa kurejea katika nafasi yake ya uongozi wa ligi baada ya kuwfunga goli 3-0 Ruvu shooting ya Pwani.
Katika mchezo huo uyliochezwa katika dimba la Azam complex lililopo Chamanzi, lilishuhudia Azam FC kwa mara nyingine wanapata goli la mapema zaidi baada ya Kipre Herman Tcheche kufunga goli lake la saba likiwa ni goli la kwanza kwa mchezxo huo katika dakika ya kwanza ya mchezo.
Tcheche alipasa mpira nyavuni kuvuatia pasi ya v iliyotlewa na chipukizu Joseph Kimwaga na kuipa Azam goli la uongozi katika dakika ya kwanza ikiwa ni sekunde 4 nyuma ya goli la John Bocco aliloifunga Yanga pale Azam FC walipokutana na yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Ruvu shooting walionekana kucheza kwa uwelewano mku7bwa sehemu ya kati ya uwanja na kupeleka Azam FC kucheza mipira mirefu na huku Ruvu shooting wakitawala mchezo lakini wakkosa maarifa ya kuweka mp9ira nyavuni.
Katika dakika 45 Waziri Salum, alipiga krosi iliyokutana na Joseph Kimwaga ambapo bila ajizi aliipatia Azam goli la pili kwa kichwa huku likiwa goli lake la pili msimu huu, la kwanza akiwafunga yanga katika ushindi wa goli 3-2. Na mchezo kwenda mapumziko kwa Aam FC wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili kilikuwa ni cha kushambuliana kwa zamu huku dakika 15 za mwanzo mchezo ulitawaliwa na Ruvu shooting lakini dakika 30 za kumalizia mchezo, Azam FC waliutawala mchezo huo.
Kazi nzuri ya Kipre Herman Tcheche katika dakika ya 70 ilii[patia Azam goli la tatu likifungwa na Khamisi Mcha akiunga mpira wa Tcheche, na kupelekea mchezo kwisha kwa azam fc kuibuka na ushindi wa goli 3-0, na kufanikwa kufkisha point 26 wakiwa sawa na Mbeya city ambapo watakutana november 7 mwaka huu.
Kikosi
cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum,
Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Khamis Mcha, Himid Mao/Jabir
Aziz dk58, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno na Joseph Kimwaga/Farid Mussa
dk69.
0 Maoni:
Post a Comment