Kipa wa mabingwa wa kombe la mapinduzi Azam FC, Aishi Salum Manula huenda akakosa mchezo kati ya Azam FC na Costal union utakaocheza siku ya jumamosi katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,
Manula ameumia katika mazoezi ya timu yake ya Azam FC, ambayo iko jijini Tanga kwa ajili ya mchezo huo wa jumamosi hii.
Manula alishindwa kufanya mazoezi leo kutokana na jeraha lake alilopata na kuongeza idadi ya majeruhi wa Azam Fc sasa kufikia watatu baada ya Himid Mao kuumia katika maandalizi ya kuelekea mchezo dhidi ya Prisons sambamba na majeruhi wa mda mrefu Samih Hajji Nuhu.
Meneja wa Azam FC amesema kuwa timu inaendelea vizuri na mazoezi jijini Tanga ambapo wanamatumaini ya kufanya vyema katika mchezo huo japo kuwa kipa wao Manula amepata jeraha kuelekea mchezo huo wa jumamosi.
Manula ambaye ametoka katika kikosi cha Azam academy na kuwa nyuma ya kipa Mwafini Ally katika msimu uliopita lakini msimu huu ameonekana kumvutia kocha Stewart Hall na kupeleka kumuweka benchi kipa Mwadini Ally katika michezo iliyopita.
Katika michezo 6 ambayo Azam FC wamecheza mpaka sasa Manula amedaka michezo 5 kati ya hiyo 6 ya lgi kuu ya vodacom.
Azam FC iko jkatika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 10 sawa na wapinzani wao wa siku ya Jumamosi Coastal union walio katika nafasi ya 4 wakiwa na pointi hizo 10.
Kocha msaadizi wa Azam FC, Kally Ongala kueleka mchezo huo wa jumamosi amesema wako Tanga kwa ajili ya kushinda na wanataraji kuondoka na pointi zote tatu katika mchezo huo wa jumamosi.
"Tuna mechi kama tatu tumetoka sare tumeshina mbili, si mda wa kupanic, bado mapema anaeongoza ana pointi 14, hivyo si mda wa kupanic kwa kila mtu, imradi tuaendelea kuchukuwa pointi na siku ya jumamosi tunataka kuchukuwa point 3". alisema Kally.

0 Maoni:
Post a Comment