![]() |
Pigo Azam; Himid Mao ameumia goti |
Kiungo Mkenya, Mieno na washambuliaji Mganda, Umony na mzalendo Bocco maarufu kama Adebayor walikuwa majeruhi kwa muda mrefu, lakini wiki iliyopita wakapona na kuanza kucheza.
Sasa kocha Muingereza, Stewart Hall amepoteza silaha yake nyingine muhimu, Himid ambaye amekuwa akiongoza safu ya kiungo tangu mwanzo wa msimu.
Mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Pamba SC ya Mwanza, Mao Mkami ‘Ball Dancer’ aliumia goti la mguu wa kulia siku mbili kabla ya mechi na Prisons mjini Mbeya.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said ameiambia BIN ZUBEIRY leo (jana) kwamba, Himid baada ya kuumia anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua uzito wa maumivu yake.
“Daktari wa timu (Mwanandi Mwankemwa) alirejea Dar es Salaam tulivyotoka Mbeya, anatarajiwa kuungana na timu tena Tanga siku ya Alhamisi na amesema akifika hapa ndipo atampeleka Himid katika hospitali ya Bombo kufanyiwa uchunguzi,”alisema Jemadari.
![]() |
Goti la Himid lililoumia |
Timu hizo ziliongozana zote Mbeya kwa mechi za mwishoni mwa wiki, Coastal ikitoa sare ya 1-1 na Mbeya City na Azam ikitoa sare ya 1-1 pia na Prisons, Uwanja wa Sokoine Jumapili.
CHANZO: BIN ZUBEIRY
0 Maoni:
Post a Comment