Na Prince Akbar, Ilala
TIMU ya vijana ya Coastala Union leo imeanza vyema michuano ya Kombe la Uhai baada ya kuwafunga Azam mabao 2-1.
Huo
ulikuwa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya vijana ‘Kombe la Uhai’ chini
ya umri wa miaka 20 uliofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Coastal
Union ilienda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Erick
Haule dakika ya tatu baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam.
Dakika
ya 50 Coastal Union ilisawazisha bao kwa njia ya penalti mfungaji
akiwa Raizin Haji baada ya beki mmoja wa Azam kuunawa mpira eneo la
hatari.
Coastal
iliendelea kufanya mashambulizi ya nguvu na dakika ya 55, Raizin Haji
alifunga Coastal bao la pili akitumia ufundi kuwatambuka mabeki wa Azam
na kuukwamisha mpira wavuni.
Washambuliaji wa timu zote walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini umaliziaji haukuwa mzuri.
Mashindano
hayo yalifunguliwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF)
Wallace Karia, ambaye aliwamwagia sifa wadhamini maji ya uhai kwa
kusaidia kuibua vipaji.
Mshambuliaji wa Azam U-20,Eric Haule (kulia) akijaribu kumpiga chenga mchezaji wa Coastal Union U-20, Nzara Ndaro (kushoto) katika mashindano ya kuwania kombe la Uhai U-20,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.Coastal Union ilishinda 2-1.
Beki wa Azam U-20,Mgaya Abdul (kulia) akijaribu kumpiga chenga beki wa Coastal Union U-20,Abdallah Wazir katika mashindano ya kuwania kombe la Uhai U-20,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.Coastal Union ilishinda 2-1.
Beki wa Azam U-20,Mgaya Abdul (kulia) akijaribu kuwapiga chenga wacheaji wa Coastal Union U-20,Abdallah Wazir (kushoto) na Raizin Haji katika mashindano ya kuwania kombe la Uhai U-20,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.Coastal Union ilishinda 2-1.
Mshambuliaji wa Azam,Jamil Mchaulo akijaribu kuwatoka wachezaji wa Coastal Union,Abdallah Wazir (kushoto) na Ally Nassor katika mashindano ya kuwania kombe la Uhai U-20,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.Coastal Union ilishinda 2-1.
Beki wa Azam U-20,Mgaya Abdul (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Coastal Union U-20,Mtenji Abano (jezi namba 3) katika mashindano ya kuwania kombe la Uhai U-20,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana,kushoto ni Mshambuliaji wa Azam,Jamil Mchaulo.Coastal Union ilishinda 2-1.
Mshambuliaji wa Azam U-20,Eric Haule (kulia) akijaribu kumpiga chenga mchezaji wa Coastal Union U-20, Abdallah Wazir (kushoto) katika mashindano ya kuwania kombe la Uhai U-20,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.Coastal Union ilishinda 2-1.
| Kocha wa Simba SC wa pili kulia, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alikuwepo na wakubwa hapo
CHANZO: BINZUBERY
|
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment