Mshambuliji toka Ivorycoast Kipre Herman Tcheche leo anatarajiqa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Azam FC katika kujikita katika uongozi wa ligi pale Azam FC watakapo wakaribisha Mbeya city council FC katika uwanja wa Azam complexs uliopo Chamanzi.
Azam inaongza ligi wa point 26 sawa na Mbeya city ambapo wote hawajapoteza mchezo wowote ule na wakitofautiana katika wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Azam na Mbeya city msimu huu ndizo timu zilizo ruhusu magol machache katika nyavu zao amapo wote wameruhusu magoli 7, lakini Azam FC ikiwapiku Mbeya city katika kuziona nyavu za wapinzani mara 20 wakati Mbeya city wakiziona nyavu za wapinzani mara 16.
Mchezo wa leo ndio mchezo utakao amua nani aongoze ligi baada ya timu zote kufungana kwa pointi katika michezo 12 iliyopita na mchezo wa leo ndio wa mwisho kwa mzunguk wa kwanza.
Kikosi cha Azam kikoteyari kwa ajili ya mchezo wa leo utakao onyeshwa na Azam TV , huku kukichochewa na urejeo wa Salum Aboubakari aliyekosa mchezo uliopita baada ya kuwa anatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.
Kocha wa Azam FC aipata kunukuliwa akikiri mchezo wa leo utakuwa mgumu kutokana na uimara wa Mbeya city.
Thursday, November 7, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment