
Azam FC leo watakuwa na mazoezi ya Asubuhi tu, huku wakitaraji kuingia kambini hapo kesho (Jumatano) kwa ajili ya maandalizi wa mchezo huo wa raundi ya kwanza.
Azam, ambao msimu uliopita pia waliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo na kufanikiwa kuishia raundi ya tatu ya mashindano hayo, wakifanikiwa kuitoa Ferroviario watamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.
Malengo ya Azam FC katika mashindano ya kombe la shirikisho mwaka huu ni kupiga hatua zaidi ya pale walipo fikia mwaka jana.
Wapinzani wa Azam FC wanataraji kuwasili nchini siku ya ijumaaa teyari kwa mchezo huo wa raundi ya kwanza ambapo Azam FC itaendelea kukosa huduma ya mfungaji bora wa wakati wote John Bocco, ambapo anataraji kurejea uwanjani wiki ijayo.
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment