Wednesday, March 19, 2014

AZAM NA YANGA NGUVU SAWA

Posted By: kj - 8:55 PM

Share

& Comment


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMwxUaJ16jR7V23HZFqVDJmKU6mDDOUyokKX1j32XN-716Uy0SF5sKQtqqKk7L-V8XZ86CsEz0QLsgL1Q0Uq1lXzuL2nR0MfoTCxYr8I63Woe15Yy-XODQP4XK1cVqKD19v8p7Z8RkCOY/s1600/KEVIN1.jpg

Kwa mara nyingine tena mchezaji chipukizi toka Azam Academy anaiwezesha Azam FC kutoka na pointi mbele ya Yanga.

Ikiwa ni baada ya chipukizi Joseph Kimwaga kuisaidia Azam FC kuichapa Yanga goli 3-2 katika mchezo wa awamu ya kwanza na leo hii chipukizi Mwingine aliyefunga goli 4 katika mchezo dhidi ya Coastal Union Kelvin Friday aliifungia Azam FC goli la kusawazisha na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.



Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Yanga walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 13 kupitia kwa Didier Kavumbagu akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aishi Salum Manula ambapo leo alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya Yanga.

Katika kipindi cha kwanza Azam FC walipoteza umakini katika upande wa ulinzi na kuwafanya Yanga kutengeneza nafasi kadhaa lakini kutokana na uimara wa Manula aliyeitwa katika timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 "Ngorngoro heroes" alifanikiwa kuondoa hatari hizo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-W1rX4mQqYJVFuNfwEIxsxJFc0twh1uBWXaMlkk2ufkPXLrS4pjkHsfUxXzYwneei372LY0FPf_s7Fbmzo04u6Gr0USb2tstF9MJWfRI0qDeCRZDDCsorX_GGGW5QqiLfXSy7TSHnpuw/s1600/_DSC0053.JPG
Kipre Herman Tcheche amanusura aipatia Azam goli la kusawazisha kufuatia shuti lake alilopiga baada ya mabekia wa Yanga kuokoa mpira wa kona kugonga mwamba na hivyo kupelekea Azam FC kwenda Mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuliandama lango la Azam FC bila mafanikio huku safu ya ulinzi ya Azam FC iliyomkosa Aggrey Morrice katika mchezo wa leo ikionekana kuimarika na pia kipa Aishi Manula akizidi kuonyesha uhodari wake katika kulinda lango.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYWXrPPMxc9I5Jmrfed1nH_LXW1H7-3o-purDLWveRZGlBBC-fjUBsvvHfFo2Tu1YNuGn4H6P75Zv8g-PnwGai1qyEhJ9tGwTN2ZmAVzK8mC_10AUCLBlf5nLZFitTkA0X5MuVXuyJ06s/s1600/_DSC0064.JPG
Kocha wa Azam FC alimpumzisha Hamisi Mcha na nafasi yake ikachukuliwa na Kelvin Friday katika dakika ya 59, mabadiliko yaliyopelekea Azam FC kurejea mchezoni.

Katika dakika ya 72 Yanga walipata penati iliyopigwa na Hamisi Kiiza, ambapo Aishi Salum Manula aliicheza penati hiyo huku kukishuhudia beki Erasto Nyoni akizawadiwa kadi nyekundu na kupelekea Azam FC kumaliza wakiwa pungufu.

Kelvin Friday katika dakiak ya 83 aliisawazishia Azam FC kwa shuti kali lililo mshinda kipa Juma Kaseja na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kwa matokeo hayo ya leo Azam FC ambayo imecheza michezo 20 bila ya kupoteza wamefikisha pointi 44 wakiwa katika kileleni mwa msimamo wakifuatiwa na Yanga iliyocheza michezo 19 wakiwa na point 40.

Azam FC leo: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mwantika, Said Moradi, Kipre Bolou, Himid Mao, Salum Aboubakari/ Raphael Bryson, Kipre Tcheche, John Bocco, Hamisi Mcha/Kelvin Friday 



0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.