Katika michuano hiyo inayoshirikisha timu nne ambazo ni TP Mazembe, Don Bosco ZESCO sambamba na Azam FC inataraji kuanza siku ya jumatano januari 29 mwaka huu.
Michuano hiyo inacheza kwa kuzikutanisha timu zote nne kwa hivyo kutoa furasa kwa kila timu kucheza michezo mitatu.
Azam FC inataraji kurejea nchini february 4 mwaka huu, na katika msafara huo utakao enda DR Congo utajumuisha wachezaji 24 ambao ni makipa Mwadini Ally, Aishi Salum, Jackson Wandwi na Khalid Mahadhi.
Mabeki ni Salum Kapombe, Agrey Morice, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, David Mwantika, Said Morad na ardiel Michael.
Viungo ni Salum Aboubakri, Mudathir Yahya, Franky Domayo, Himid Mao, Amri Kiemba, Kipre Bolue na Khamis Mcha.
Washambuliaji ni Kelvin Firday, John Bocco, Brian Majegwa, Gaudency Mwaikimba, Dider Kavumbagu na Kipre cheche.
0 Maoni:
Post a Comment