Katika mchezo huo wa leo ambao Azam fc walikuwa ndio wenyeji japokuwa ulichezwa katika uwanja wa Taifa, ulishuhudia shabiki wa Azam Steve kulilia akiondolewa katika jukwaa la upande ambao umezoeleka kukaliwa na yanga na alipokwenda upande mwingine ambao unakaliwa na simba sc aliondolewa pia, ikiwa kabla ya mchezo kuanza.
Simb sc walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Emanuel Okwi katika dakika ya 17 ya mchezo akipiga shuti lililo mshinda Mwadini Ally na kupelekea simba sc kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha kwanza azam fc walicheza vyema katika eneo la kati ya uwanja, na kupelekea simba sc walazimike kupitia pembeni mwa uwanja katika kutengeneza nafasi ambapo walitengeneza nafasi moja wakati azam fc wakitengeneza nafasi 4 na kushindwa kuzitumia.
Katika dakika ya 50 Franky Domayo alikwenda benchi na nafasi yake ikachukuliwa na Khamis Mcha, John Bocco aliingia kuchukuwa nafasi ya Kavumbagu katika dakika ya 53.
Katika dakika ya 57 krosi ya Mcha ilimkuta Tcheche na bila ajizi aliisawazishia azam fc na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika dakika ya 70 Emanuel Okwi aligongana na Agrey Morice na kupelekea Okwi kupoteza fahamu na kutolewa uwanjani na kukimbizwa hosipitalini.
Kutolewa kwa Okwi kuliliweka lango la simba katika wakati mgumu baada ya azam fc kuongeza mashambulizi bila mafanikio.
0 Maoni:
Post a Comment