Katika mchezo huo ambao Kagera sugar waliuwanza kwa kasi ya chini na kupelekea azam fc kupata goli la mapema katika dakika ya 2 kupitia kwa Kipre Herman Tcheche akiitumia vyema pasi ya Mudathir Yahya.
Goli hilo lilipelekea kwa kagera sugar kutulia na kuanza kupasiana katika eneo lao na kupeleka mipira mirefu ambayo liliishia kwa walinzi wa azam fc, na Kagera sugar kushindwa kuliweka katika misukosu lango la azam fc katika kipindi chote cha kwanza.
Katika dakika ya 36 Didier Kavumbagu aliiandikia azam fc goli la pili akiunga krosi ya Kipre Tcheche na kuipeleka azam fc mapumziko waliwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili kagera sugar walirejea kwa kasi na kuipa misukosuko lango la azam fc kwa dakika 5 za mwanzo na katika dakika ya 48 Rashid Mandawa alifanikiwa kuwafungia Kagera sugar goli pekee katika mchezo huo.
Kuingia kwa goli hilo kulipekea kocha Omog kumpumzisha Franky Domayo na nafasi yake kuchukuliwa na Himid Mao ambaye aliituliza azam fc na kupeleka mashambulizi kadhaa langoni mwa Kagera sugar.
Dakika 62 Didier Kavumbagu aliipatia azam fc goli 3 akiunga mpira wa kona uliopigwa na Brian Majegwa na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam fc kwa ushindi wa goli 3-1 na kufikisha pointi 20 ambazo zinawaweka kileleni mwa ligi.
0 Maoni:
Post a Comment