Saturday, January 17, 2015

AZAM FC WAKALIA USUKANI, WAICHAPA STAND GOLI 1

Posted By: kj - 7:46 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPtz0GrRTQXFCQU7CXCWbQvOOTei5CcFXMLH8Tnb08OIrYedZ-yavhyOP-vecFOogJHN0Swry_urjZsxQkrRBgH5zY1m0KrJPAU9w9WFBP6E0VFahP77wzQuw0A4qi6_3GRj7MHaFDW4AG/s320/10920903_891901590850198_6678503210394433039_n-709727.jpg
Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Azam FC hii leo wameibuka na ushindi wa goli 1-0 na kupanda hadi kwenye uongozi wa ligi wakitokea katika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

Azam FC hii leo walikuwa katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakiwa wa geni wa Stand United katika muendelezo wa ligi kuu ya vodacom.


Katika mchezo huo ambao Stand united waliuwanza kwa kucheza kwa uwelewano katika eneo la kati ya uwanja kabla ya viungo wa Azam FC kulirejsha kwenye himayo yao katika dakika ya 30 na kuutawala mchezo kitendo kilicho wapelekea Stand united kutumia mipira mirefu kupandisha mashambulizi.

Azam FC iliwabidi wa ngoje mpaka dakika ya 45 kupata goli pekee la ushindi kupitia kwa Azam Fc lilifungwa na Franky Domayo aliyepiga shutia kali ambalo kipa wa Stand United aliudumbukiza mpira nyavuni.

Katika mchezo wa leo kama Didier Kavumbagu na Kire Tcheche wangwkuwa makini Azam FC wangeshinda zaidi ya goli 3 huku Gadiel Michael akipoteza nafasi nzuri katika kipindi cha pili,

Brian Majegwa naye alipoteza nafasi katika kipindi cha pil akiwa natazamana na kipa wa Stand united kabla ya Himid Mao Mkame kupiga shuti afifu alipowekea pasi muruwa na Kapombe ambapo kipa aliudaka.

Stand United nayo ilitengenea nafasi tatu ambzo zingewazawadia magoli katika mchezo wa leo lakini walisshindwa kiztumia.

Azam FFC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morice, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Mudathir Yahya/Himid Mao, Franky Domayo/Kipre Bolue, Didier Kavumbagu/Mwaikimba, Kipre Tcheche, Brian Majegwa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.