Friday, January 9, 2015

KILICHOANDIKWA KWENYE UKURASA WA AZAM BAADA YA KUTOLEWA MAPINDUZI CUP

Posted By: Unknown - 8:47 AM

Share

& Comment

Kama klabu, tunazipongeza JKU na Mtibwa Sigar kwa kushinda na kutinga Nusu Fainali.... Mliokuwa mnatulazimisha tufukuze kocha anzeni kufukuza kocha wenu. Sisi hatuwezi fukuza kocha kwa sababu timu haichezi soka lake tulilozoea, tunajua kuwa moyo wa timu yetu ni kiungo... Tunacheza na viungo ambao ni kama wapya kwenye timu (Domayo, Mudathir, Majwega na wakati mwingine Erasto) tunawapa muda makocha wetu, tunajua wanaona matatizo na wanayafanyia kazi.

Wakati mwingine timu hupita kwenye kipindi kigumu cha majeruhi na kupoteza mtiririko wake.... Katika kipindi kama hiki, muhimu kama timu ni kukaa pamoja, kujadili matatizo yetu pamoja na kuyafanyia kazi.
Tunaendelea kuipongeza Mtibwa Sugar na sisi tunabeba changamoto na kuzifanyia kazi.

Tutasafiri hadi Lubumbashi DRC kucheza na Zesco, TP Mazembe na Don Bosco katika kuendelea kuiandaa timu. Tumepania kufanya vema Afrika na tuna imani na makocha wetu.

Kama walifanya vizuri wakiwa na KCCA na AC Leopards kwa nini wasirudie mafanikio hayo wakiwa na sisi.
Azam FC, Tucheze pamoja kwa furaha

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.