Thursday, February 28, 2013

KALLI AOMBEWA KUKAA BENCHI,

Posted By: azam fans - 8:57 AM

Share

& Comment

Kocha msaidizi wa azam fc Kally Ongala ameombewa na uongozi wa azam fc kwa shirikisho la soka nchini TFFlimruhusu kukaa kwenye benchi ya timu hiyo wakati wanaendelea kuchunguza vyeti vyake.

Ongala aliziuiwa na TFF kukaa kwenye benchi la azam mpaka watakapo maliza kupitia vyeti vyake vilivyowasilishwa katika ofisi za TFF.

Katibu mkuu wa azam fc Nassoro Idrissa alisema kuwa wameamua kuiandikia barua ya kuwaomba TFF wamruhusu Ongala kukaa kwenye benchi wakati uchunguzi juu ya vyeti vyake ukiendelea.

"Ongala alifungiwa lakini tulishapeleka vyeti vyake muda mrefu lakini mpaka sasa wamekaa kimya hivyo tumewaandikia barua ya kumruhusu kocha huyo msaidizi mpaka pale watakapojiridhisha na uchunguzi wao," alisema Nassoro Idrissa.

Uongozi wa azam fc wamefikia hatua hiyo baada ya kocha wao mkuu Stewart Hall kufungiwa kwa michezo mitatu ya ligi kuu ya vodacom pamoja na kutozwa faini ya Tsh 500000 kwa kosa ya kutooa bukta yake katiki mchezo dhidi ya Kagera sugar uliochezwa katika uwanja wa azam complex.



--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.