Friday, February 22, 2013

NGOMA KUCHEZWA TAIFA KESHO, UMONY NA BOLOU NDANI

Posted By: azam fans - 9:44 PM

Share

& Comment

Masikio na macho ya mashabiki wa soka la bongo kesho yataamia taifa kushuhudia mabingwa wa mapinduzi azam fc wakichuana na mabingwa wa kombe la kagame yanga wakichuana kusaka kiti cha uongozi wa ligi kuu ya vodacom.

azam kesho itakuwa na nyota wake wote ukiwaondoa Uhuru Selemani na Samir Haji Nuhu walio majeruhi, huku Kipre Bolou na Brian Umony walio umia katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya al-nasri, wako fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Kocha wa azam fc Stewart Hall amesema kuwa urejeo wa Umonyi na Bolou ni chachu kwa wachezaji wengine kuelekea mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom.

Azam na yanga zote zinapoint 36 yanga ikiizidi azam katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa, huku azam wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Kiburudisho katika mchezo wa kesho utakuwa namna viungo Salum Aboubakary 'Sure boy' na Haruna Niyonzima 'Fabrigas' watakavyokuwa wanachezesha timu zao hapo kesho.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.