Samih alipata jeraha hilo la mgongo katika mchezo wa kirafiki kati ya azam na simba uliochezwa jumatatu asubuhi katika uwanja wa azam uliopo Chamanzi na azam kuibuka na ushindi wa goli 3-1.
Samih atakuwa nnje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja na ataanza kwa kukosa mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya mtibwa sugar utakao fanyika katika uwanja wa Manungu complex.
Samih aliyerejea katika uwanja msimu huu baada ya kuwa majeruhi kwa msimu mzima msimu uliopita wa 2011/12 baada ya kuumia katika duru la pili msimu wa 2010/11 na katika msimu huu alirejea kwa kasi na kurejesha namba yake iliyokuwa inashikiliwa na Waziri Salum akisaidiana na kiraka Erasto Nyoni.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment