Saturday, February 23, 2013

YANGA YAICHAPA GOLI MOJA AZAM

Posted By: azam fans - 7:32 PM

Share

& Comment

Yanga hii leo wamejikita kileleni baada ya kuwachapa azam fc goli 1-0, katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa taifa.

Azam wakicheza bila ya mshambulhaji wake toka Uganda Brian Umonyi nusura wapate goli la kuongoza katika dakika ya 4 kupitia kwa Kipre Tchetche, ikiwa ni kabla ya Jerry Tegete kupoteya nafasi alipo kutana na kipa wa azam Mwadini Ally.

Katika dakika 30 za mwanzo mchezo ulikuwa sawa huku wakipeana zamu katika kushambuliana ambapo shambulizi la dakika ya 31 lilizaa goli kwa yanga, goli liliko fungwa na kiungo Haruna Niyonzima akipokea pasi toka kwa Jerry Tegete.

Kuingia kwa goli hilo lilipelekea mchezo kuamia kwa azam fc lakini wakishindwa kutemgeneza nafasi za wazi na katika dakika ya 34 John Raphael Bocco alifunga goli lililoktaliwa na mwamuzi kwa madai ya Bocco kumcheza faulo kipa wa yanga Ally Mustapha na Bocco akazawdiwa kadi ya njano kwa kitendo cha kumzonga mwamuzi.

Yanga nusura waandike goli la pili na la tatu katika dakika ya 41 na 44 kupitia kwa Tegete aliyepoteza nafasi zote na kupelekea mchezo kwenda mapumziko yanga wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa upande wa azam ambapo Himid Mao aliingia kuchuka nafasi ya Ibrahim Mwaipopo mabadiliko yaliyopelekea Michael Bolou kurejea katika nafasi yake ya kiungo cha ukabaji na kupelekea azam kuendelea kupandisha timu bila mafanikio.

Yanga waliwapumzisha Hamisi Kiiza na Jerry Tegete na kuwapisha Said Bahanuzi na Didier Kavumbagu huku azam wakiwapumzisha Michael Boloue nafasi ikachukuliwa na Jabir Azizi na Mcha Khamisi akimpisha Abdallah Seif.

Mabadiliko hayo haya kuweza kubadili matokeo na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kufungwa goli 1-0 ukiwa mcheyo wa tatu mfululizo kwa azam kupoteya mbele ya yanga.

Baada ya dakika 90 kumalizika wachezaji wa azam walhenda kumzonga mwamuzi kitendo kilicho pekelekea mwamuzi kuondolea na askari wakio kuwewepo uwanjani hapo.


[MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15]

AZAM EC LEO:
MWADINI ALLY
MICHAEL BOLOU/JABIR AZIZI
WAZIRI SALUM
JOACKINS ATUDO
DAUD MWANDIKE
IBRAHIM MWAIPOPO/HIMID MAO
KIPRE TCHETCHE
HUMPHREY MIENO
JOHN BOCCO
SALUM ABOUBAKARI
KHAMISI MCHA/ABDALLAH SEIF

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.