Azam fc ambayo imeingia kambini leo kwa ajili ya maandalizi wa mchezo huo utakaochezwa kati ya machi 16 na 17 pamoja na mchezo wa ligi kuu ya vodacom utakao chezwa jumamosi machi 9 katika uwanja wa azam.
Katibu mkuu wa azam fc Nassoro Idrisa ameiomba shirikisho la soka Tanzania TFF kusogeza mbele michezo miwili ya azam fc ya ligi kuu ya vodacom utakao chezwa jumatano (machi 13)na ule wa jumamosi (machi 16).
"Jumatano (machi 13) ndiyo siku ambayo tunatarajia kuondoka hapa kwenda Liberia na ukiangalia kwenye ratiba ya ligi kuu tutakuwa tuna mecgi na jumamosi (machi 16) ambayo tutakuwa tayari Liberia gia tumepangiwa kucheza. Sasa tunaiomba TFF isogeye mbele mechi hizo mbili ili tupate fursa nzuri ya kujipanga kwa mtihani huu wa kuiwakilisha nchi." alisema Nassoro Idrissa..
Nassoro aliongeza kuwa kikosi chake kina majeruhi mmoja kwa sasa ambaye ni Samir Hajji Nuhu, huju wakitaraji kuwaacha wachezaji watatu pamoja na Nuhu katika msafara huo, wengini watakao achwa ni beki Omari Mtaki pamoja na kipa Mwandi.
Wachezaji wanaotaraji kusafiri kwa mujibu wa Nassoro ni; makipa MWADINI ALLY, AISHI MANUELA
mabeki ni JACKSON ATUD6, DAVID MWANTIKA, HIMID MAO, WAZIRI SALUM, MALIKA NDEULE, LACKSON KAKOLAKI
viungo ni KIPRE BOLOU, JABIR AZIZI, IBRAHIM MWAIPOPO, SALUMA ABOUBAKARI, HUMPHREY MIENO, KHAMISI MCHA, UHURU SULEIMAN, ABDI KASSIM, ABDULHALIM HOMOUD.
washambuliaji ni JOHN BOCCO, KIPRE TCHETCHE, SEIE ABDALLAH, GAUDENCE MWAIKIMBA, BRIAN UMONY
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment