Tuesday, April 9, 2013

AGREY ARUDISHWA KUNDINI

Posted By: kj - 5:40 PM

Share

& Comment

Beki wakutumainiwa wa Timu ya taifa, Taifa stars Agrey Morice amerejeshwa ndani ya kikosi cha azam fc kinachojiandaa na mchezo dhidi ya African lyon utakao chezwa april 11 mwaka huu.

Uongozi wa azam fc uliwasimamisha wachezaji wa nne ambao ni Agrey Morice, Erasto Nyoni, Deogratius Munish na Saidi Moradi kwa tuhuma ya rushwa iliyoshindwa kuthibitishwa na taasisi ya kuzuia rushwa nchini 'TAKUKURU'.

Azam fc iliwasimamisha wachezaji hao ili kuwapa uwepesi TAKUKURU katika upelelezi wa tuhuma hizo za kupokea rushwa ili wapange matokeo katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya simba sc.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa azam fc Nassor Idrissa inaeleza kuwa TAKUKURU imewakuta wachezaji hao hawana hatia.

"AZAM FC inatoa taarifa rasmi kuwa TAKUKURU haijawakuta na hatia ya rushwa wachezaji; DEOGRATIUS BONIVENTURE MUNISHI, ERASTO NYONI, SAID HUSSEIN MORAD NA AGREY MORRIS." ilieleza taarifa hiyo.

Nassor Idrissa aliongeza ndani ya taarifa yake ya leo april 9 kuwa wachezaji hao wanatakiwa kujiunga na kikosi cha azam fc kwa ajili ya kumalizia michezo iliyo salia.

"Hivyo wachezaji hao wanakaribishwa rasmi kurudi kikosini AZAM FC kwa ajili yakujiunga na mazoezi na wachezaji wenzao." ilieleza taarifa ya Nassor Idrissa.

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.