Monday, April 8, 2013

KAHEMELE; HATUNA SHIDA KWA WAPINZANI KUSHANGILIWA

Posted By: kj - 12:22 PM

Share

& Comment

Wawalishi wa Tanzania katika kombe la shirikisho azam fc wamesema hawana shida na kitendo cha baadhi ya mashabiki wanaofika katika uwanja wa Taifa kwa dhumuni ya kuwashangilia wapinzani wao kama ilivyotokea katika michezo dhidi ya Barack yc na Al nasri Juba.

Akizungumza na clouds fm meneja wa azam fc Patrick Kahemele amesema hawana shida na mashabiki wanao fika katika uwanja wa taifa kwa dhumuni ya kuwashangilia timu pinzani zinazocheza dhidi yao.

Kahemele amewashukuru mashabiki wanavyo zidi kujitokeza katika michezo yao ya kimataifa, akisema mashabiki ni moja ya sehemu ya mchezo bila kujali wako katika upande wako ama la.

Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Al nasri uliomalizika kwa azam kushinda goli 3-1 ulishudiwa na mashabiki elfu 13 wakati mchezo wa pili dhidi ya Barack yc uliomalizika kwa sare ya bila kufungana ulishuhudiwa na mashabiki zaidi ya elfu 14 na kukusanywa milioni 44.

Azam fc wanataraji kuwa karibisha AS FAR RABAT ya Moroco april 19-21 katika uwanja wa Taifa na kurejeana kati ya mei 2-4 nchini Moroco ikiwa ni michezo ya raundi ya pili ya kombe la shirikisho.

Akizungumzia mchezo huo Kahemele amesema watajiandaa vyema na mchezo huo na kuendeleza kuwapa burudani watanzania na kuwakilisha vyema Tanzania katika michuano hiyo.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.