Katika mchezo huo wa leo Barack YC II waliweza kuwadhibiti viungo wa azam fc katika kipindi cha kwanza kitendo kilichopelekea washambuliaji wa azam kukosa mipira ya uhakika katika kipindi cha kwanza huku mchezo ukitawala kwa kupokezana.
Katika kipindi cha kwanza kipa wa azam fc Mwadini Ally hakudaka mpira wowote wa maana huku kipa wa Barack YC akiwa na kazi ya ziada ya kuokoa hatari 3 kati ya nafasi 4 walizopoteza azam fc katika kipindi cha kwan9a kupitia kwa Mieno na Kipre Tchetche.
Mshambuliaji toka Uganda Brian Umonyi leo alishindwa kuonyesha cheche zake na katika kipindi cha pili alipumzishwa na nafasi kuchukuliwa na Khamisi Mcha Viali.
Katika kipindi hicho cha pili mchezo uliendelea kutawaliwa kwa zamu na safari hii Barack walifanikiwa kufika langoni mwa azam na kushindwa kutia mpira kimiani.
Kipre Bolou amanusura aipatia goli azam fc baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kubaki na kipa ila mpira alioupiga ulipaa juu ya lang6.
Azam fc walizidi kutengeneza nafasi za magoli lakini wakishindwa kuzitumia nafasi hizo, huku wakishindwa kupiga pasi nyingi kama walivyozoeleka, na mwisho wa mchezo azam fc 0-0 barack yc.
Azam wamewatoa Barack yc kwa jumla ya goli 2-1 waliyoyapata katika mchezo wa awali, huku AS FAR wanayokutana nayo katika hatua ya pili wakiwatoa Al nasri ya Libya kwa jumala ya goli 2-1.
Azam fc leo: MWADINI ALLY, HIMID MAO, WAZIRI SALUM, JACKSON ATUDO, DAVID MWANTIKA, MICHAEL BOLOU, KIPRE TCHETCHE, SALUM ABOUBAKARY, JOHN BOCCO, HUMPHREY MIENO/ABDALLAH SEIF NA BRIAN UMONYI/ KHAMISI MCHA.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
0 Maoni:
Post a Comment