Mshambuliaji toka Ivorycoast anaecheza katika klabu ya azam fc, Kipre Herman Tchetche jana amefikia idadi ya magoli aliyoyafunga Mrisho Khalfan Ngassa ndani ya msimu mmoja akiwa na uzi wa azam fc, huku akibakiwa na magoli matatu kufikia rikodi ya mshambuliaji wa timu yake John Bocco.
Bocco anashikilia rikodi mbili ndani ya klabu ya a9am fc ambazo ni ufungaji bora wa wakati wnte wa klabu pamoja na kuwa mchezaji aliyeifungia magoli mengi azam fc katika msimu mmoja wa ligi kuu ya vodacom ambapo alifanya hivyo katika msimu wa 2011/12 akifunga magoli 19.
Kipre Tchetche jana alifunga magoli mawili katika ushindi wa goli 3-1 walio upata mbele ya Afrika lyon na kufikisha magoli 16 katika msimu huu.
Katika mchezo huo wa jana uliochezwa azam complex azam fc walikuwa wa mwanzo kuziona nyavu za wapin9ania wao katika dakika ya 10 kupitia kwa Khamis Mcha kabla ya Tchetche kufunga goli mbili katika dakika ya 28 na 61.
Goli pekee la lyon lilifungwa na Adam Kingwande katika dakika ya 36 na kupelekea azam kuibuka na ushindi wa goli 3-1 na kufikisha pointi 46 wakiwa nyuma kwa point 3 zidi ya vinara wa ligi hiyo yanga.
Msemaji wa azam fc, Japhari Iddi Maganga akizungumzia mchezo baada ya kumalizika amesema azam walistahili ushindi huo, na wapinzani wao walicheza vizuri.
."Kipindi cha kwanza kiukweli Lyon walitulia na
kucheza vizuri, lakini kipindi cha pili tuliwazidi sana na tume washinda kwa halali, sasa hesabu zetu ni mnyama Simba ambaye tunakumbana naye mwshoni mwa wiki
hii" alisema Idd.
"Si kazi nyepesi,kila mtu amejipanga barabara dakika hizi zalala salama, lakini tuna timu nzuri inayoweza kushindana, sasa kocha wetu anajipanga upya kwa ajili ya Smba ambayo imejaza vijana waliotufunga siku za nyuma" aliongeza Idd.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment