Azam fc waliingia kambini jana kwa ajili ya mchezo huo ambao wakipata sare wanajihakikishia nafasi ya pili ya ligi kuu ya vodacom na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho mara mbili mfululizo.
Mgambo shooting wakiwa katika nafasi ya 11 na wamejikusanyia pointi 25 wanahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo huo, kujihakikishia ubakiji wake katika ligi kuu ya vodacom.
Msemaji wa azam fc, Japhari Iddi Maganga amesema timu imeingia kambini jana na wachezaji wote wamerejea katika hali yao ya kawaida baada ya kuadhiriwa na mchezo dhidi ya AS FAR Rabat wa kombe la shirikisho ambapo azam fc walifungwa goli 2-1 na kutolewa katika michuano hiyo.
Akielezea hali ya John Bocco (mchezaji aliyeripotiwa kuadhiriwa zaidi na matokeo ya mchezo huo), Maganga alisema nae yuko sawa kwa sasa na anaendelea vyema na amekubaliana na kilichotokea katika mchezo huo.
0 Maoni:
Post a Comment