[pichani Kipre Tchetche akishangilia goli la tatu. picha na Bin Zubeiry]
Azam fc leo wameendeleza wimbi lao la kupata ushindi wa si chini ya goli 3 katika uwanja wake wa Azam complex toka mzunguko wa pili uanze na timu iliyonusurika na kichapo cha goli 3 katika mzunguko huu ni Polisi moro pekee, ambao walitoa sare ya goli 1-1.
Azam fc waliandika goli la kwanza kupitia kwa John Raphael Bocco akiunga mpira wa Humphrey Mieno katika dakika ya 25 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa azam fc kuwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha pili Azam fc walifanikiwa kuandika goli la pili kupitia kwa Kipre Tchetche na Tchetche kujihakikishia kiatu cha dhahabu katika msimu huu baada ya kufikisha magoli 17, na ikiwa msimu wa tatu mfululizi mfungaji bora wa ligi kuu kutoka katika kikosi cha azam fc.
Goli la tatu na la mwisho kwa Azam fc lilifungwa na Humphrey Mieno akiunga kwa kichwa kona iliyopigwa na Erasto Nyoni na kuifanya Azam fc kufikisha point 51, ambazo haziwezwi kufikiwa na simba sc yenye pointi 45.
0 Maoni:
Post a Comment