Wednesday, August 28, 2013

AZAM KUWAKABILI RHINO LEO

Posted By: Unknown - 12:40 AM

Share

& Comment

Picha zote kutoka katika blog ya BIN ZUBEIRY

Mabingwa wa kombe la mapinduzi Azam FC leo wanataraji kutupa karata ya pili ya ligi kuu ya vodacom pale watakapo kuwa wageni wa Rhino Rangers katika uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Azam wakitokea kutoa sare ya goli 1-1 na Mtibwa sugar wataendelea kukosa huduma za kinara wa kufumania nyavu katika historia ya Azam FC John Raphael Bocco aliyeumia katika mchezo wa ngao ya hisani uliochezwa katika uwanja wa taifa dhidi ya Yanga.

Nnje ya Bocco Azam FC pia wataendelea kukosa huduma ya mshambuliaji toka Uganda Brian Umonyi na kiungo kutoka Kenya Humphrey Mieno waliokuwa bado majeruhi, na huenda wakamkosa mshambuliaji Abdallah Seif Karnihe.

Azam FC jana walifanya mazoezi mepesi katik uwanja wa Ally Hassan Mwinyi yakiwa ya kuelekea mchezo huo wa leo dhidi ya Rhino walio lazimisha sare ya goli 2-2 kwa Simba SC.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.