Wednesday, August 28, 2013

AZAM WAKUMUTA RHINO GOLI 2

Posted By: Unknown - 7:32 PM

Share

& Comment

Magoli ya Gaudence Mwaikimba na Abdallah Seif Karinhe hii leo yameipatia Azam FC point tatu na kuwafanya wa pande mpaka katika nafaci ya tatu wakilingana point naYAnga, coastal union na Simba SC wakipishana katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Azam FC leo walikuwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora wakiwa wamekaribishwa na wanajeshi Rhino Ranger ya mkoani hapo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Azam FC waliutawala mchezo huo na dalili ya ushindi zilianza kuonekana mapema baada ya Kippre Tchetche na Khamisi Mcha kupoteza nafasi kadhaa katika kipindi hicho cha kwanza.

Kocha Stewart Hall alilazimika kufanya mabadiliko asiyo ya kusudia baada ya mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kuumia na nafasi yake kujazwa vyema Abdallah Seif Karinhe katika kipindi hicho cha kwanza.

Azam FC waliandika goli lake la kwanza kwa shuti kali la Gaudence Mwaikimba katika dakika 55 baada ya dakika 45 za mqwanzo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kuingia kwa goli hilo liliwaduliza wachezaji wa Azam FC waliokuwa wanasaka goli la kuongoza kwa udi na uvumba na kuanza kuwapa burudani mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo huku wakiwa wanasaka goli la pili.

Kijani aliyekulia katika kituo cha Orange Academy kilichopo Zanzibar kabla ya kujiunga na academy ya Azam FC Abdallah Seif Karinhe kuandika goli la pili kwa Azam FC katika dakika ya 79.

Azam fc hii leo:  Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Jackson Atudo, Aggrey Morrice, Boluo Michael, Jabir Azizi, Salum Aboubakari, Gaudence Mwaikimba, Khamisi Mcha, Kipre Tchetche/Abdallah Seif

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.