Saturday, September 14, 2013

AZAM WATOA SARE NA KAGERA

Posted By: Unknown - 7:55 PM

Share

& Comment

Azam FC leo wamefanikiwa kutoka na point moja kwenye uwanja wa Kaitaba baada ya kwenda sare ya goli 1-1 na watumiaji wa uwanja huo Kagera sugar.

Kagera Sugar ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Themi Felix katika kipindi cha kwanza akiunga mpira wa kona, na kupelekea Azam FC wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili Azam FC walisawzisha goli hilo kuptia kwa Kamisi Mcha na kupelekea Azam FC kuvuna pointi moja katika uwanja wa huo, ambao ni mgumu kwa Azam FC.

Azam FC imefanikiwa kutoka na point zote tatu katika uwanja wa Kaitaba katika ziara zote walizo zifanya katika uwanja huo, ambapo walivuna point huizo tatu msimu uliopita kwa ushindi wa goli 1-0.

Azam FC baada ya kucheza michezo mitatu nnje ya Daer es salaam, itarejea rasmi katika uwanja wake wa Azam complex uliopo Mbagala Chamanzi hapo agosti 18 watakapo wakaribisha Ashanti united.

Azam FC wamefanikiwa kuvuna point tano mpaka sasa ambapo wamefanikwa kupata ponti moja katika uwanja wa Manungu (Mtibwa sugar) na Kaitaba (Kagera sugar) na kuchukuwa point 3 katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi (Rhino ranger)

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.