Wednesday, September 18, 2013

ASHANTI YAIKOMALIA AZAM FC

Posted By: azam fans - 6:28 PM

Share

& Comment

Makamu bingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam Fc mambo hii leo yaliwaendea kombo baada ya kulazimishwa sare na Ashanti united katika uwanja wake wa manjinjio (Azam complex) na kufikisha pointi 6.

Azam FC leo waliuanza mchez vyema na mnamo dakika 20 waliandika goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake toka Ivory coast Kipre Tchetche na kuwaamsha Ashanti united.

Safu ya ushambuliaji ya Ashanti united liyokuwa inaongozwa na Said Maulidi iliisumbuwa ngome ya Azam FC na kupelekea kufanya madhambi mara kwa mara katika ngome yao.

Pamoja na Ashanti kuonyesha mchezo mzuri hii leo lakini walishindwa kuziona nyavu za Azam katika kipindi cha kwanza ambacho mchezo ulikwa sawa huku timu zikishambuliana kwa zamu.

Kipindi cha pili kocha wa Azam FC Stewart Hall alianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumpumzisha Jabir Azizi na nafasi yake kuchukuliwa na JOhgn Raphael Bocco, mabadiliko yaliyo ongeza presha langoni mwa Azam FC.

Kuonekana kushindwa kwa presha ya Ashanti united kulipelekea mlizi Aggrey Morice kuzawadiwa kadi nyekundu na kupelekea kocha Stewart Hall kumtoa GAudence Mwaikimba na nafasi yake kuchukuliwa na David Mwantika.

Kadi hiyo nyekundu iliyo tolewa katika dakika ya 67 ilizidi kuipa nguvu Ashanti United na kuendelea kulisakama lango la Azam FC na mnamo dakika ya 79 wakafanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Antony Matangalu.

Kama Ashanti United wangetulia zaidi walikuwa na uwezo wakupata goli la pili na kuibuka na ushindi wa kwanza tangu ligi ianzae lakini wameishia kuambulia sare yao ya kwanza hii leo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.