Wednesday, September 18, 2013

AZAM WAREJEA CHAMANZI, LEO KUWAFUNDISHA SOKA WAUZA MITUMBA

Posted By: azam fans - 8:00 AM

Share

& Comment

Timu bora ya Azam fc leo wanarejea katika uwanja wake wa nyumbani uliopo Chamanzi pale watakapo wakaribisha Ashanti united "wauza mitumba wa Ilala" katika muendelezo wa ligi kuu ya vodacom.

Mchezo wa leo ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom kwa Azam fc kucheza katika uwanja wa azam complexs baada ya kuwa katika uwanja wa Manungu complex, Ali Hassam Mwinyi na Kaitaba.

Katika viwanja hivyo Azam fc wameambulia point 5 inayomuweka katika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom

Katika mchezo wa leo dhidi ya Ashanti united inayoshika nafasi ya mwisho, huenda kukarhuhudia urejeo wa kinara wa mabao ndani ya Azam fc, John Raphael Bocco ambaye ajaonekana uwanjani toka msimu uwanze.

Wachezaji wengine waliokuwa majeruhi Brian Umonyi na Humphrey Mieno nao huenda wakapata dakika katika mchezo wa leo, wakati Samih Haji Nuhu akiendelea kuuguza jeraha lake.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.