Sunday, September 22, 2013

AZAM NA YANGA TAIFA LEO

Posted By: azam fans - 1:31 AM

Share

& Comment


Azam FC leo watashuka uwanja wa Taifa kuwakabili mabingwa wa tetezi wa ligi kuu ya vodacom Yanga katkamuendelezo wa ligi kuu ya vodacom.

Azam FC na yanga wanakutana wote wakiwa na point sawa na wakiwa wamecheza michezo sawa ambapo kila mmoja  amecheza michezo minne na kukusanya point 6.

Azam na yanga wote wametoka sare mara tatu mfululizo na mara mbili kati ya hizo tatu wamezipata mikoani na hivyo kutoa taswira ya kuwepona mchezo wa kuvutia na msisimko hi leo jioni katika uwanja wa TAifa.

Yanga na Azam mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni wa ngao ya jamii uliochezwa katika uwanja wa Taifa mwezi uliopita na yanga wakitoka uwanjani na ushindi wa goli 1-0.

Toka mchezo a ngao ya jamii mshambuliaji wa Azam FC John Raphael Bocco anaetarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji hii leo alikuwa nnje ya uwanja na alianza kuonekana katika mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Ahanti akitokea benchi kuchukuwa nafasi ya JAbir Azizi mchezo uliomalizika kwa sare ya goli 1-1.

Wakati Bocco akipewa nafasi kubwa ya kuanza hii leo, waliokuwa majeruhi wenzake Humphrey Mieno na Brian Umonyi huenda wakaendelea kutoonekana uwanjani katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom.

Katika kipindi hiki cha mwakaq mmoja Azam FC wamekuwa na matokeo mabaya mbele ya Yanga ambapo wamejikuta wakipoteza mchezo kila wanapo kutana nao.

Azam FC hii leo watakuwa na kibarua cha kufuta uteja ka Yanga huku wakisaka point tatu muhimu zitakazo wasogeza karibu na kinara wa ligi kuu ya vodacom Simba SC wenye point 11.

Katika vitu vilivyo inyima Azam FC ubingwa msimu ulopita ni kushindwa kupata matokeo katika mechi 4 walizo cheza katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.