Sunday, September 22, 2013

KUMWAGA AMDHIHIRISHIA HALL HAKUFANYA KOSA KUMPA JEZI LEO, AZAM WAKIICHAPA 3-2 YANGA

Posted By: azam fans - 6:19 PM

Share

& Comment

Joseph Kumwaga leo amewapa Azam furaha waliyoikosa kwa takribani miaka miwili baada ya kuiwezesha Azam FC kutoka na ushindi wa goli 3-2 mbele ya YAnga.

Joseph ni mchezaji wa Azam Academy aliyeingia kip[indi cha pili kuchukuwa nafasi ya chipukizi mwenzake wa Azam Academy Farid Mussa MAlik wote wakiwa wanaichezea Azam FC kwa mara ya kwanza.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa TAifa Azam FC waliandika goli la kwanza kupitia kwa John Raphael Bocco katika dakika ya kwanza ya mchezo goli lililo waamsha Yanga na kuanza kulishambulia lango la Azam FC bila mafanikio katika kipindi chote cha kwanza.

Azam FC walicheza vyema katika kipindi hicho cha kwanza lakini muda mwingi walijikuta wakicheza katika eneo lao na kuokoa hatari za YAnga.

Katika kipindi cha pili YAnga walirejea kwa kasi na katika dakika ya 49 walisaazisha goli kupitia kwa Didier Kavumbagu ikiwa ni baada ya John Bocco kuwakosa yanga na Yanga wao pia kukosa goli kuvuatia Jackson Atudo kuondosha mpira uliokuwa unaelekea langoni mwa Azam FC.

Goli hilo liliwarejesha yanga mchezoni na kuanza kushambuliana kwa zamu ndipo mtokea Benchi Hamisi Kiiza Diego alipoiandikia Azam goli la pili katika dakika ya 66.

Mabadiliko aliyoyafanya kocha Stewart HAll ya kumuingiza KIpre Herman Tcheche kuchukuwa nafasi ya Brian Umonyi yalipelekea Azam FC kuongeza presha langoni mwa Yanga  na katika dakika ya 68, bekii wa Yanga Nadir HAroub aliushyika mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penati kwa AZam Fc.

Penati hiyo iliyosababishwa na Kipre Tcheche, ilitiwa kimiani na Kipre Herman Tcheche katika dakika ya 69 na kupelekea kasi ya mchezo kunogezeka.

Kukionekana kuzidiwa kwa mbinu kwa kocha wa Azam FC aliamua kumuingiza chipukizi Joseph Kumwaga kuchukuwa nafasi ya Farid Mussa, na mashabiki kufikri ndio mwisho wa zam FC katika mchezo wa leo ambapo Aishi MAnula aliokoa hatari nyingi golini mwake.

Joseph KUmwaga alikifanya kile anachokifanya katika timu ya vijana ya Azam FC (Azam Academy) kwa kuipachikia Azam FC goli  la ushindi katika dakia za nyongeza na kuifanya Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 3-2.

Joseph Kusaga ni mchezxo wake wa kwanza kuichezea Azam FC na amefasnikiwa kufunga goli lake la kwanza ndani ya kikosi cha Azam FC,

Azam FC Leo: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, JOacksen Atudo, Himid MAo, Kipre Bolue, Humphrey Mieno, John Bocco, Brian Umonyi/Kipre Tcheche, Farid Musa MAlik/Joseph Kumwaga
DAKIKA 83: AZAM FC 2-2 YANGA (J.BOCCO 2'K.Tcheche 71p', D.Kavumbagu 49' H.Kiiza 67) 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.