Kocha Msaidizi
wa Azam FC, Kally Ongala amesema wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya
kukabiliana na wapinzani wao Tanzania Prisons.
Azam
wanatarajiwa kuvaana na Prisons keshokutwa Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu
Bara mechi itakayochezwa kwenye Uwanja Sokoine Mkoani Mbeya.
Kocha huyo
alisema kuwa kikosi kipo fiti kwa ajili ya mechi hiyo, hivyo mashabiki
watarajie kupata matokeo mazuri.
“Wachezaji
wote wana afya njema na wapo tayari kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wetu,
hivyo mashabiki watarajie kupata matokeo mazuri kutokana na maandalizi
tuliyofanya,” alisema Ongala.
0 Maoni:
Post a Comment