Mshambuliaji wa timu ya Azam pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa anatajiwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya mpambano dhidi ya Manchester united. Ngassa ametajwa kwenye kikosi cha Seattle Sounders ambacho kitacheza na Manchester United hapo julai 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Taarifa zilizo wekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Azam fc, Ngassa atacheza mchezo huo kama sehemu ya majaribio katika klabu hiyo ya Marekani. "Ngassa kuchezea Seattle Sounders Vs Manchester United july 20 ambapo pia Seattle watatumia fursa hiyo kumjaribu. Mchezaji hahitajii kucheza mechi za kimataifa kupata nafasi ya kwenda majaribio. mchezaji anahitaji klabu makini kama Azam FC" maneno toka kwenye kurasa wa Azam fc.
Hii ni mara ya pili kwa Ngassa kupata nafasi ya kujaribiwa, baada ya majaribio ya mwanzo aliyo yafanya katika klabu ya WestHam united ya Uingeleza iliyoshuka daraja msimu uliokwisha na kushindwa kupata nafasi.
Mrisho Ngassa amepata kuwa sumbua mabeki wanaotamba ulimwenguni kwa nyakati tofauti akiwa amevaa uzi wa Taifa stars, na kufikia hatua ya kocha wa Arsenal, Arsen Wenger kumfananisha na Walcot katika mpambano baina ya Brazil na Tanzania. Mabeki waliokutana na kimbembe cha Ngassa ni pamoja na Mcameroun Alexandre Song anae kipiga Arsenal, Kole Toure anayecheza Manchester City, wabrazil Juan na Bastos.
Ngassa pia alipata bahati ya kutaka kusajiliwa bila majaribio na klabu inayoshiriki ligi kuu ya Norway lakini yanga walikataa Ofa hiyo wakati Ngassa alipokuwa anakipiga Yanga.
Mrisho Ngassa ataungana na Nizar Khalfan kucheza na timu toka jiji la Manchester zinazo tamba ligi kuu ya Uingeleza. Timu ya Nizar, Vancouver Whitecaps inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na Manchester City hapo baadae.

0 Maoni:
Post a Comment