Thursday, February 9, 2012
ITC ya Bolou yatua, kucheza dhidi ya Simba
Posted By: kj - 5:51 PMKiungo mshambuliaji toka Ivory Coast Kipre Bolou Michael Wilfried anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom, february 11 wakati Azam FC watakapo alikwa na Simba katika uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook, zinasema kuwa Bolou amepata ITC yake ambayo ilikuwa ikimkwamisha kucheza michezo ya ligi kuu ya vodacom.
"Mchezaji wetu Kipre Bolou Michael Wilfried ambaye ITC yake ilichelewa kutua nchini imewasili leo. Hivyo basi Kipre Bolou atashuka dimbani kwa mara ya kwanza kwenye mechi za ligi kuu dhidi ya Simba SC jumamosi hii. Shukrani kwa wote waliofanikisha mchakato huu hasa watu wa FIFA, TFF na Chama cha soka cha Ivory Coast," ilieleza taarifa hiyo.
Kipre Bolou, Salum Abubakar Sure Boy, Abdulhalim Homoud pamoja na Abdi Kassim Babi walitengeneza Chemistry nzuri katika michezo ya kujipima nguvu na ile ya Mapinduzi ambapo Azam FC hawakupoteza mchezo wowote ule, huku wakiwachapa Simba na Yanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment