Thursday, June 16, 2011

Mshambuliaji anaeye chukiwa na usimba na uyanga

Posted By: azam fans - 10:12 AM

Share

& Comment

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Jan Paulsen amesema, John Bocco ndiye mshambuliaji bora kabisa wa kati wa Tanzania kwa sasa.

Paulsen ameendelea kusema, Tuna bahati ya kuwa na Samata ambaye ana uwezo mkubwa wa kucheza nyuma ya mshambuliaji kwa ufasaha mkubwa sana na John Bocco ni wa kipekee kabisa kwani ni #9 aliyekamilika. Lakini tatizo la Stars linakosa viungo ( mabega) ya kupeleka cross zenye akili. mabeki wa pembeni na washambuliaji wa pembeni (mawinga) ndilo tatizo kubwa la Stars.

Paulsen amesema eneo la golikipa, mabeki wa kati na viungo wakabaji lipo vizuri lakini anapotafuta viungo washambuliaji na mabega (wa pembeni) hapo ndipo kwenye tatizo kwani mara nyingi washabuliaji hukosa mipira yenye akili wafanye kazi ya kumalizia.

Kwa kauli hiyo Paulsen anaungana na makocha wengine wakigeni Marcio Maximo, Itamar Amorim na Stewart Hall ambao wote wanaamini kuwa Bocco ndiye mshambuliaji bora wa Tanzania kwa sasa (ingawa hali ni tofauti kwa mashabiki).

katika mechi kati ya Stars na South Africa, licha ya mashabiki kumkataa boko lakini wakala kutoka Afrika ya kusini bwana Kimesh Gladis (Glades) alionesha kuvutiwa na Bocco na akasema "The boy can do better in PSL, keep me informed on his development, we may do business in the next few month.

Statistics pia zinamsaidia Bocco ambaye amekuwa mfungaji bora namba mbili msimu wa pili mfululizo VPL.


Chanzo: post ya Patrick Kihemela katika Kandanda group.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.