Wednesday, July 6, 2011

Kikosi B cha Azam FC kushiriki michuano ya Rollingstone

Posted By: kj - 12:49 PM

Share

& Comment

Kikosi cha pili cha Azam FC kinatarajiwa kushiriki michuano ya vijana chini ya miaka 20 inayo andaliwa na kituo cha michezo cha Rolling stone.

TIMU 20 za vijana chini ya miaka 20, zimethibitisha kushiriki mashindano ya soka ya Afrika ya Mashariki na kati yanayoandaliwa na taasisi ya kuibua na kukuza vijana ya Rolling stone ya Jijini Arusha.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi julai 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid yata shirikisha pia timu tano kutoka nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa mashindano hayo, Bille Mwilima alisema kuwa timu kutoka nje ya nchi ambazo zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ni pamoja na Kenya, Burundi, Congo, Rwanda na Uganda.

Mwilima alizitaja timu za Tanzania ambazo tayari zime kubali kushiriki mashindano hayo ambayo mwaka huu yatakuwa na ushindani wa hali ya juu ni pamoja na Bingwa mtetezi timu ya Simba B, Yanga B, Azam B, Ruvu Shooting B na Oljoro JKT B ya Arusha inayoshiriki kwa mara ya kwanza.

Mwilima alizitaja nyingine ni pamoja na Zanzibar Kaskazini na Zanzibar Magharibi, Don Breakers ya Dar es salaam, timu ya Saadani ya mkoani Pwani, timu ya Mbeya Art, Street Children na Tea ya Mkoani Mwanza na Tanga Yorth na Kong Hearald za Jiji Tanga na Twalipo na Hananasifu za jijini Dar es salaam.

Mratibu huyo alizitaja timu za mkoa wa Arusha zilizo thibitisha kushiriki mashindano hayo ni pamoja na Flamingo, Rolling stone, Jamhuri, CDTI na Bishop Durning.


source mwananchi

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.