MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Ngassa anayechezea klabu ya Azam FC anaondoka leo kuelekea Marekani tayari kwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Seattle Sounders.
Akizungumza na Mwananchi mratibu wa safari hiyo, Rahim Kangezi alisema maandalizi yote yamekamilika na kesho (leo) Ngassa ataondoka kuelekea Marekani tayari kwa majaribio.
Kangezi alisema baada ya majaribio hayo, Ngasa ataichezea timu ya Seattle Sounders itakapocheza na Manchester United hapo Julai 23 ambayo itakuwa ni mechi ya kirafiki, hivyo kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza dhidi ya mabingwa hao wa England.
Kangezi alisema majaribio ya mchezaji huyo mahiri wa Taifa Stars yatafanyika mapema kabla ya Julai 13 kama ilivyotangazwa hapo awali. Alisema wanatarajia Ngasa atafanya vizuri katika majaribio hayo ikiwa ni sambamba na kufanya vema katika mechi ngumu dhidi ya Mashetani hao Wekundu ambao watakuwa na ziara nchini Marekani.
Wakati mwananchi ikiripoti habari ya Ngassa, kwa upande wa pili kiungo wa kimataifa wa Tanzania Jabir Azizi bado haja pata kibali cha kuingia nchini Norway.
Friday, July 8, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment