Friday, September 30, 2011

AZAM HII NI TOFAUTI NA ILE ILIYOPITA.

Posted By: kj - 10:44 AM

Share

& Comment

Ligi kuu Tanzania Bara imesimama kupisha michezo ya kufuzu kusaka nafasi ya kucheza Mataifa ya Africa.

Mpaka sasa kila timu imecheza michezo 8 huku Azam ikiwa katika nafasi ya pili wakiwa na point 15, baada ya kufungwa mchezo mmoja toka sare mitatu na kushinda minne, wakati nyavu za Azam zikichunguliwa mara mbili na wakifunga magoli 6 katika michezo hiyo 8.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Azam FC kuruhusu idadi ndogo ya magoli ya kufungwa na kufunga idadi ndogo ya magoli tangu ishiriki ligi kuu ya Vodacom katika msimu wa 2008/09.

Hii ni Tathmini fupi ya kikosi cha Azam FC ndani ya michezo hiyo nane iliyocheza.

MAKIPA.

Azam FC wamefanya usajili wamaana katika eneo hili ambapo Mwadini Ally na Obren Cuckovic walisajiliwa huku Daudi Mwasongwe akipandishwa kuchukua uzoefu toka kwa makipa hao.

Mechi tatu za Mwanzo alidaka Obren Cuckovic na kuruhusu magoli 2 katika michezo hiyo ambapo Azam FC walishinda mchezo mmoja, kufungwa mmoja na kutoka sare mmoja.

Obren aliumia kidole na kumpatia nafasi ya kudaka Mwadini Ally ambapo alianza na mchezo dhidi ya Simba na kufanikisha kucheza michezo mitano bili ya nyavu zake Kuguswa.

Kipa huyo toka Mafunzo ya Zanzibar aliwakuna mashabiki wa soka la bongo katika mchezo dhidi ya yanga na kupelekea mashabiki kumshangilia kila alipo okoa hatari za Yanga. Kiwango chake ndani ya michezo mitano imezua kizaazaa kwanini hayumo kwenye kikosi cha Taifa stars kinacho jianda na mchezo dhidi ya Morocco.

MABEKI.

Moja ya sababu ya Azam FC kucheza michezo 8 wakiruhusu goli 2 ni ukuta uliopo chini ya beki wazamani wa Ashanti, Simba na Kagera Sugar Said Morad na kijana toka visiwani Zanzibar Aggrey Morrise.

Ukuta huu ndio bora kwa sasa kuliko ule wa Victor Costa na Juma Nyosso ambao umesharuhusu goli 4 mpaka sasa. Morrise na Morad wanapata msaada wakutosha toka kwa mabeki wapembeni Erasto Nyoni na Waziri Omary Salum.

Partiner ya Morad na Morisse imemfanya Mghana Nafiu Awudu kusota bench, huku kijana toka Mafunzo Waziri Omar kumepelekea kapteni Ibrahim Shikanda kuanzia benchi na kucheza dakika chache mpaka sasa.

Shikanda alikuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Azam ambapo nafasi yake imezibwa vyema na chipukizi huyo.

Erasto Nyoni alipotea katika siku za karibuni na kujikuta akipoteza nafasi katika timu ya Taifa, lakini msimu huu karejea vyema na kumshawishi kocha wa stars kumita kikosini.

VIUNGO.
Ukitaja viungo vilivyo onyesha kiwango cha juu mpaka sasa utoacha kulitaja jina la kiungo Ibrahim Mwaipopo. Mwaipopo alipata nafasi ya kuanza kufuatia kadi nyekundu ya Salum Abubakari 'Sure boy' katika mchezo wa pili dhidi ya African lyon ambapo Azam FC walilala goli moja lililo fungwa na chipukizi toka Azam Academy Omega Semi.

Mwaipopo ameonyesha kiwango cha juu katika utoaji wa pasi zenye macho na katika ukabaji huku mipira yake ya adhabu kuleta kidhadhaa kwa lango la mpinzani.
Mwaipopo alishirikiana vyema na viungo ambao wanavutia kuwatizama wakiwa na mpira Jabir Azizi Stima na Ramadhan Chombo Redondo.

Abdulhalim Homoud hakupata nafasi ya kudhihirisha ubora wake kutokana na jeraha alilolipata ambalo limemuweka nnje ya uwanja, huku chipukizi Himid Mao akiachiwa ajiandae na mitiani wakati Gulam Abdallah akishindwa kupata nafasi.

Azam FC wamekuwa wakimiliki zaidi nafasi ya kati huku pasi zao za mauzi zikitoa burudani kwa mashabiki wanao hudhuria michezo yao.

USHAMBULIAJI.

Toka Azam FC ianze kushiriki ligi kuu safu ya ushambuliaji huwa inaondoka na magoli ya kutosha, ambayo huongozwa na John Bocco ambaye amesha funga goli 5 ndani ya michezo 8 aliyecheza huku chipukizi Khamisi Mcha ambaye alingara kwa kutikisa nyavu katika michezo ya preseason bado ajapata goli katika michezo minne aliyo cheza.

Mrisho Ngassa mpaka sasa ajapata goli ndani ya michezo 6 aliyocheza, huku Kipre Tchetche akiwa kaiona nyavu mara moja kati michezo mitano aliyocheza kabla ya kupata jeraha.

Jamal Mnyate bado ajapata nafasi ya kucheza, huku Mghana Abdul Wahab Yahya akitoka patupu ndani ya dakika alizopatiwa na Kocha Stewart Hall sawa na Zahoro Pazzi.


AZAM FC WATACHEZA MCHEZO WAO WATISA OKTOBA 15 MWAKA HUU DHIDI YA JKT RUVU KATIKA UWANJA WA AZAM.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.