Sunday, October 9, 2011

Gulam aendelea vyema

Posted By: kj - 11:27 AM

Share

& Comment

Mchezaji Abdulghan Gulam Abdallah wa Azam FC, amesikitishwa na kitendo cha kukosa mechi za ligi kuu kutokana na kupata majeraha siku chache kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.

Gulam alipata ufa katika kidole gumba cha mguu wa kulia wakati wa maandalizi ya ligi kuu msimu huu na kupelekea kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili na nusu.

Akizungumza na tovuti ya www.azamfc.co.tz Gulam alisema kutocheza muda wote huo kumempa unyonge kwa kuwa alihitaji kuonyesha uwezo wake pamoja na kutoa mchango katika timu yake.

“Kutocheza hata mechi moja kunanisononesha kila wakati na kufanya niwe mnyonge, nimeathirika kisaikoligia kwa kuwa timu imeshacheza mechi nane na sijacheza hata moja kutokana na maumivu yanayonikabili” alisema Gulam.

Gulam aliongeza kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri, ameshaanza mazoezi takribani wiki tatu zilizopita lakini bado anasikia maumivu kwa mbali yanayopongua kidogo kidogo.

Akielezea kurejea uwanjani Gulam alisema, anaamini kiwango chake hakijashuka hivyo atakaporejea uwanjani uwezo wake utakuwa mzuri na kutoa mchango wake kwenye timu, endapo ataendelea vizuri anatarajia kurejea uwanjani wiki mbili zijazo.

Akizungumzia ligi inayoendelea alisema ligi ni ya ushindani kila timu imejiandaa hivyo wachezaji wanatakiwa kujituma zaidi ili kupata ushindi.

Gulam amesajiliwa akitokea kwenye Klabu ya Malindi ya visiwani Zanzibar lakini tangu asajiliwe hajacheza hata mechi moja ya ligi kuu ya Tanzania bara kutokana na jeraha hilo.



Azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.