Mtibwa Sugar leo wamefanikiwa kutoka na point tatu mbele ya Azam katika uwanja wa Manungu kwa mara ya kwanza ambapo John Bocco alishindwa kumalizia mchezo.
Azam FC waliingia katika uwanja wa Manungu kuendeleza ubabe kwa Mtibwa Sugar katika uwanja uliozungukwa na miwa na kuambulia kichapo cha goli moja bila.
Katika mchezo huo Mshambuliaji hatari wa Azam FC anaeongoza katika utikisaji wanyavu John Bocco Adebayor aliumia katika dakika ya 38 na nafasi yake kuchukuliwa na Kipre Tcheche.
Kwa matokeo hayo Azam FC inasalia katika nafasi ya 3 akiwa nyuma kwa point 6 dhidi ya vinara Simba, huku wakiwa pointi sawa na yanga.
Azam wanaelekea ukanda waziwa kwa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu kwa kucheza na Kagera Sugar pamoja na Toto Africa, ambapo msimu uliopita walitoka mikono mitupu, huku wakicheza bila ya Bocco ambaye huenda akakosekana tena katika ziara hiyo.
Azam FC hii leo: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morise, Said Moradi, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakari 'sureboy', Jabir Azizi, John Bocco, Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo Redondo
Tuesday, October 25, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment