Mfungaji bora wa Msimu uliopita Mrisho Khalfan Ngassa hii leo kafanikiwa kufunga goli lake la pili, wakati kipa Mwadini akiruhusu nyavu zake kuguswa kwa mara ya kwanza.
Azam FC hii leo waliwakarimu maafande toka Dodoma, Polisi Dodoma katika uwanja wa Azam magoli matatu kwa moja.
Kipa wa Zanzibar Heroes na Azam FC Mwadini leo alicheza mchezo wake wa saba wa ligi kuu ya Vodacom na kuruhusu nyavu zake kuguswa baada ya kucheza michezo 6 bila kuruhusu goli katika nyavu zake.
Ilikuwa ni siku nyingine ya Mrisho Khalfan Ngassa baada ya kufunga tena goli la mapema ikiwa ni dakika ya pili ya mchezo. Goli hilo lilikuwa la pili kwa mshambuliaji huyo mwenye kasi, ambapo goli lake la kwanza alifunga dhidi ya JKT Ruvu dakika ya kwanza na mchezo.
Utasema nini juu ya John Bocco Adbayor ambaye kwa sasa ndie nembo ya Azam na anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi klabuni hapo. Tangu msimu huu uanze pale Azam wanapotoka na goli lazima nae awe miongoni mwa waliocheka na nyavu.
Leo Bocco alifunga goli lake la saba na likiwa la pili kwa Azam FC hii leo, wakati goli la tatu likifungwa na Ramadhani Chombo Redondo.
Redondo alifunga goli lake la kwanza na hivyo Azam wakisogea mpaka nafasi ya pili wakiwa na point 21 nyuma kwa point tatu za viongozi Simba.
Azam FC hii leo; Mwadini, Erasto, Shikanda, Moradi, Aggrey, Mwaipopo, Sureboy, Jabir Aziz, John Bocco, Redondo, Ngassa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment