Wednesday, December 14, 2011
Azam kujipima na Yanga kuchangisha pesa kukomboa viti maalum
Posted By: kj - 9:35 PMJeshi la Azam FC lilipo katika machimbo ya Chamanzi nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam wanatarajiwa kusogea mpaka mitaa ya uwanja wa Taifa december 20 kujipima nguvu na Yanga katika mchezo maalum wakuchangisha pesa za kukomboa viti vya walemavu vilivyokwama bandarini.
Viti hivyo vya walemavu vimekwama katika bandari ya Dar es Salaam, baada ya kukosekana ushuru wa kuvilipia, ambavyo vinatoka nchini Marekani vilipotumwa na shirika moja lisilo la kiserikali.
Katika kuimarisha kikosi cha Azam FC wameongezwa wachezaji watatu wapya ambao ni Abdi Kassim Babi, Kipre na Joseph Owino.
Kikosi cha Azam FC wanaendelea kujifua katika kiwanja chake kilichopo Chamanzi kwa ajili ya duru la pili ya ligi kuu ya Vodacom.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment