Sunday, December 25, 2011
Obrean kutimkia Vietnam
Posted By: kj - 3:52 PMKipa wa Azam FC toka nchini Serbia, Obren Cirkovic ameondoka nchini na kwenda Vietnam kucheza
soka la kulipwa katika klabu ya Hoang Anh Gia Lai.
Obren, aliyesajiliwa na Azam mwanzoni mwa msimu pamoja na Kipa toka Zanzibar Mwadini Ally kuchukua nafasi ya makipa Chove na Nyokururu toka Burundi ameenda nchini Vitenam wakati bado Azam FC na Hoang Anh Gia Lai bado hawajafikia makubaliano ya bei.
Gazeti la Champion liliripoti kuwa Obren kauzwa kwa kitita cha dola za Marekani 25,000, ambapo walimnukuu Kocha wa Azam FC Stewart Hall akikisema kiasi hicho cha pesa.
“Tayari Azam imeshakubaliana na klabu hiyo juu ya dau litakalomng’oa kipa huyo, Hoang Anh Gia Lai, ambapo watalazimika kulipa dola 25,000 (zaidi ya Sh milioni 40) ili kumpata kipa huyo," alisema Stewart Hall.
Ila kwa mujibu wa taarifa toka mmoja ya watu wa ndani ya Azam FC, inasema kuwa bado hawaja wafikiana kwenye kitita cha fedha japo kuwa teyari ameshaondoka.
Obrein ambaye alidaka michezo mitatu ya mwanzo wa msimu na kupata jeraha ambalo lilimfanya Mwadini Kumpoka namba, pengo lake linatazamiwa kuzibwa na kipa bora wa michuano ya Uhai Cup 2011 iliyomalizika kwa Azam Academy Kushika nafasi ya pili, Aishi Salum.
Kocha Stewart akizungumzia hali yakuondoka kwa kipa huyo aliyeanza kulizoea benchi alisema: “Tumeshaanza maisha mapya bila yeye ambapo nafasi yake nimempa Aishe (Salum) ambaye alikuwa katika kikosi chetu cha vijana chini ya miaka 20, nadhani atatusaidia akiwa chaguo la pili nyuma ya Mwadin (Ali).”
Azam FC walibakiwa na makipa wawili baada ya kipa aliyelelewa na klabu hiyo Daudi Mwasongwe kutolewa kwa mkopo kwenda Villa Squad na hivyo kumpa nafasi Aishi kuwa chaguo la tatu kabla ya Obrein kutimka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Obren katika harakati ya kuokoa katika moja ya mechi alizopata kuidakia Azam
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment