Tuesday, February 7, 2012
Azam yavunja rikodi zake
Posted By: kj - 12:03 AMAzam FC baada ya kushuka uwanjani kwa mechi 16 za ligi kuu ya vodacom na kubakisha michezo 10 kumaliza msimu wameweka rikodi zifuatazo ndani ya klabu hiyo yenye maskani Chamanzi.
POINTI 32 KATIKA MICHEZO 16
Azam FC imefikisha pointi 32 baada ya kushuka dimbani mara 16 ikiwa ni rekodi kwa Azam FC tangia ianzishwe.
Pointi 32 ni ziada ya pointi tisa (9) walizozipata msimu wa kwanza baada ya kupanda daraja kwani Azam FC ilimaliza ligi ikiwa na pointi 23 msimu huo huku ikiepuka kutokushuka daraja. Ligi ilikuwa na michezo 22.
Pointi 32 ni pungufu kwa pointi mbili katika msimu uliofuatia wa 2009/2010 kwani Azam FC licha ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu lakini ilimaliza na pointi 34, pointi 20 Nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba ambao walimaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote wakiwa na pointi 54. Katika msimu huo pia Azam FC ilishuka dimbani mara 22.
Katika msimu uliopita wa 2010/2011, Azam FC ilimaliza msimu ikiwa na pointi 40, kwa hiyo hivi sasa Azam FC ipo nyuma kwa pointi nane (8) licha ya kucheza michezo 16 tuu, michezo sita nyuma ya michezo ambayo Azam FC walicheza msimu uliopita uliokuwa na michezo 22.
BOCCO NA MAGOLI 11
Mshambuliaji John Raphael Bocco anaongoza mbio za kusaka kiatu cha dhahabu akiwa amefunga magoli 11 katika mechi 16.
Msimu wa 2009/10 kiatu cha dhahabu kilienda kwa Mussa Hassan Mgosi baada ya kufunga magoli 14, Bocco alimaliza na magoli 12, idadi ambayo alimaliza nayo mwaka jana ambapo kiatu cha dhahabu kilitwaliwa na Mrisho Ngassa.
Magoli 11 katika mechi 16 huku kukiwana na mechi 10 mkononi msimu huu kunatoa picha kwamba Bocco anaweza kuvunja rekodi yake na ya VPL ambayo inashikiliwa na Boniface Ambani na Mohammed Husein Mmachinga wote kutoka Yanga ambao waliwahi kufunga magoli 18 msimu mmoja.
MAGOLI MACHACHE YA KUFUNGWA
Azam FC hadi sasa imeruhusu magoli sita tuu na kuweka rekodi ya msimu, Ligi Kuu na kwa klabu pia. Ukuta uliotengeneza rekodi hii ni Aggrey aliyecheza dakika 1430, Said Moradi aliyecheza dakika 1380, Erasto Nyoni aliyeshuka dimbani dk 1290, Waziri Salum 1296, Mwadini Ally 1170, Obren Curkovic dk 270, Ibrahim Shikanda 282, Haji Nuhu dk 44 na Luckson Kakolaki dk 16.
Golikipa Mwadini Ally ambaye amefungwa magoli manne hadi hivi sasa naye amefikisha mechi ya tisa (9) pasipo kufungwa msimu huu.
Msaada wa azamfc.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment