Saturday, March 10, 2012

Azam waichapa yanga, na kukalia usukani wa ligi

Posted By: kj - 9:05 PM

Share

& Comment


Azam FC leo wamefanikisha kufikisha pointi 41 katika msimu huu wa 2011/12 kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa klabu ya Azam FC, huku wakikaa katika usukani wa ligi mpaka kesho ambapo Simba watawakaribisha Toto Africa katika uwanja wa Taifa. Azam FC wameichapa Yanga goli 3-1 hii leo.

Katika mchezo huo wa Ligi kuu ya Vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Azam walianza kuhesabu magoli katika dakika ya 4 kufuatia goli la Mshambuliaji hatari wa Azam John Bocco Adbayor.

Goli hilo la mapema liliwashtua Yanga na katika dakika ya 12 na 14 walishuhudia kiungo wa kimataifa toka Rwanda Haruna Niyonzima na beki Nadir Haroub wakizawadiwa kadi nyekundu, ikiwa ni kadi ya pili za njano kwao.

Kadi nyekundu hizo zilimpelekea kocha wa Yanga Kostadin Papic kufanya mabadiliko kwa kumtoa Davis Mwape na Kuingia Chacha Marwa na dakika ya 24 alimtoa Shamte Ally na kuingia Godfrey Bonny.

Yanga walirejea mchezoni baada ya goli la Hamisi Kiiza katika dakika ya 30 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa upande wa Azam FC ambapo AbdiKasim 'Babi' alichukua nafasi ya Ibrahim Mwaipopo. Na katika dakika ya 54 kiungo toka Ivory Coast Michael Bolou alifunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya Vodacom na kuipa uongozi Azam FC wa goli 2-1.

John Bocco alirudi tena nyavuni katika dakika ya 76 akifunga goli lake la 15 katika msimu huu, na kubakisha goli moja kufikia rikodi ya mshambuliaji Mrisho Ngassa ya kuifungia Azam FC magoli 16 katika msimu mmoja, Ngassa alifanya hivyo katika msimu uliopita.

Goli la Bocco lilipelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kushinda goli 3-1. Kwa ushindi wa leo Azam wamekaa kileleni kwa mda uku wakivunja rikodi zake kwa kufikisha point 41 na kuwa mchezo wa 4 kuifunga Yanga mfululizo.


Walio wakilisha Azam FC Leo: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Moradi, Aggrey Morisi, Kipre Bolou, Mrisho Ngasa, Salum Abubakary 'sure boy'/Abdulhalim Homoud, Ibrahim Mwaipopo/Abdi Kassim, John Bocco/Mwaikimba, Kipre Tchetche.

Walio wakilisha Yanga leo: Shaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Stephane Mwasika, Nadir Haroub Cannavaro, Athuman Iddi Chuji, Nurdin Bakari, Shamte Ally/Godfrey Bony, Haruna Niyonzima, Davis Mwape/Chacha, Hamisi Kiiza, Omega Seme

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.